19 Juni 2026 - 16:48
J.D. Vance: Trump Ndiye Mshirika Pekee Mwenye Nguvu wa Israel

Makamu wa Rais wa Marekani, J.D. Vance, amesema Rais Donald Trump ndiye mshirika pekee mwenye nguvu wa Israel kwa sasa, akiwataka viongozi wa Tel Aviv kuacha kuikosoa Washington huku akisisitiza kuwa sehemu kubwa ya silaha za Israel hutolewa na Marekani kwa fedha za walipa kodi wa Marekani.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA - Makamu wa Rais wa Marekani, J.D. Vance, amewakosoa baadhi ya mawaziri wa serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, walioikosoa makubaliano ya Washington na Tehran, akisema kuwa Rais Donald Trump ndiye mshirika pekee mwenye nguvu ambaye Israel amebaki naye kwa sasa.

Vance alisema kuwa, iwapo angekuwa sehemu ya Baraza la Mawaziri la Israel, asingemshambulia kisiasa mshirika huyo pekee mwenye ushawishi mkubwa duniani ambaye bado anaonyesha uungaji mkono kwa Israel.

Aidha, alisisitiza kuwa sehemu kubwa ya silaha zinazotumiwa na Israel hutolewa na Marekani na kugharamiwa kupitia kodi za walipa kodi wa Marekani, akionya kuwa viongozi wa Israel wanapaswa kuthamini uhusiano wao na Washington badala ya kuushambulia hadharani.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha